Mwanamke mmoja nchini Kenya anatuhumiwa kumuua na kumzika mtoto wa siku moja baada ya kulaumiana na mume wake juu ya kupata mimba nje ya ndoa

Mume wa mwanamke huyo amekuwa mbali na mkewe kwa majukumu ya kikazi kwa zaidi ya mwaka na alishangazwa kusikia mkewe anatarajia kujifungua ambapo alimpigia simu kufahamu hilo

Mwanamke huyo aligundulika na shemeji yake ambaye alimripoti na walipombana alisema kuwa amemzika mtoto huyo kwenye shamba la mihogo, lililokuwa karibu na nyumbani kwao

Mtoto huyo amezikwa kwa mara ya pili kwa heshima, na mwanamke huyo amekimbia baada ya kujua kuwa anatafutwa