Mshambulaji Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Inter Milan bao la pili dakika ya 21 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen kwenye mchezo wa mkondo mmoja wa Robo Fainali ya UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Merkur Spiel-Arena Jijini Dusseldorf, Ujerumani. Bao la kwanza la Inter Milan lilifungwa na Nicolo Barella dakika ya 15, wakati la Bayer Leverkusen lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 24 na sasa kikosi cha Antonio Conte kitakutana na mshindi kati ya Shakhtar Donetsk na Basel zinazomenyana leo katika Nusu Fainali Jumapili