Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama amesema,

”Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras  mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota Bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kuripuka na kusababisha apoteze maisha”.

Polisi inahusisha uwepo wa Bomu hilo katika kijiji hicho huenda ni kilikuwa kikitumiwa kama njia na makundi ya waasi waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda kambi ya wakimbizi ya Mtabila hivyo kudhaniwa huenda liliangushwa na watu hao.

Jeshi la polisi imetoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea.

View this post on Instagram

—————————————————————Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020. Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama amesema, ''Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras  mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota Bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kuripuka na kusababisha apoteze maisha''. Polisi inahusisha uwepo wa Bomu hilo katika kijiji hicho huenda ni kilikuwa kikitumiwa kama njia na makundi ya waasi waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda kambi ya wakimbizi ya Mtabila hivyo kudhaniwa huenda liliangushwa na watu hao. Jeshi la polisi imetoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea. (📹 via Eatv.tv) written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Kigoma : Mtoto wa darasa la pili mwenye umri wa miaka 9 alipukiwa bomu (+Video) appeared first on Bongo5.com.