Vikosi nchini Mali vimemuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keïta na kutangaza azma yao ya kuunda serikali ya mpito kabla ya uchaguzi mpya.

Hii inakuja baada ya rais Keïta kuonekana kwenye televisheni akisema kuwa amejiuzulu.

Yeye na waziri mkuu walisindikishwa kwa mtutu wa bunduki kutoka mji mkuu Bamako hadi kwenye kambi ya jeshi.

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wamepinga kuchukuliwa kwa uongozi wa nchi na jeshi la Mali.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za magharibi, Ecowas, lilitangaza kufunga mipaka nanchi hiyo na imesitisha uhusiano wa kifedha nanchi hiyo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana baadae Jumatano.