Rais wa Iran Hassan Rouhani ametishia kuwepo na madhara iwapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa literefusha marufuku ya silaha dhidi ya Iran kwa shinikizo la Marekani.

Iran's Hassan Rouhani urges regional powers to 'unite against US ...

Rouhani amesema kupitia televisheni ya taifa, kwamba azimio nambari 2231 la Umoja wa Mataifa, ambalo ni sehemu ya makubaliano ya nyuklia yaliofikiwa mjini Vienna mwaka 2015, linahitaji marufuku hiyo iondolewe ifikapo mwezi Oktoba.

“Hivi sasa Wamarekani wamependekeza azimio dhidi ya sehemu ya azimio nambari 2231 ili kulikiuka. Tuna matumaini makubwa kwamba Marekani itashindwa”.

”Tuna matumaini makubwa tena, kwamba Marekani itagundua kushindwa kwake na kushuhudia kutengwa kwake,” amesema Rouhani.

Marekani ilijitoa kwenye makubaliano hayo Mei 2018, na baadae utawala wa Trump ukaiwekea Iran vikwazo zaidi.

Makubaliano hayo yamekabiliwa na kitisho cha kuvunjika, kwa sababu mataifa yaliosalia – China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Ujerumani, hayawezi kutekelekeza sehemu ya kiuchumi ya makubaliano kukiwa na vikwazo vya Marekani, hali iliyoisukuma Tehran pia kuanza kuyakiuka.

The post Iran yatishia kuchukua hatua, kisa Marekani appeared first on Bongo5.com.