Mwanamuziki nchini Iran, Mehdi Rajabian anakabiliwa na mashtaka kwa kosa la kufanya kazi na waimbaji na wachezaji muziki wa kike.
Mwanamuziki huyo, 30 ambaye alishawahi kufungwa gerezani mara mbili kwa kesi iliyohusu kazi zake za muziki, amesema alikamatwa majuma mawili yaliyopita.
Albamu yake, ambayo bado haijkamilika , inatarajiwa kuhusisha waimbaji wa kike, ambao wamepigwa marufuku nchini Iran.
Wizara ya utamaduni na miongozo ya Uislamu haijaongelea lolote kuhusu suala hilo.
”Utawala huu unataka kuifunga sauti yangu ,” Rajabian ameiambia BBC.” Wanasisitiza niache kupiga muziki.”
Mwanamuziki huyo aishie mjini Sari, Kaskazini mwa Iran, amesema kuwa aliitwa na vikosi vya polisi tarehe 10 mwezi Agosti, ambao walimkamata na kumpeleka mahakamani.
Mwisho wa Instagram ujumbe, 1

Rajabian amesema jaji amesema kuwa kazi yake ya sasa ”inachochea ukahaba”. Aliachiwa huru kwasababu familia yake iliweza kulipa dhamana.
”Ikiwa nitatengeneza muziki, wataondoa dhamana yangu” alisema mwanamuziki huyo. ” Ninapaswa kusubiri siku ya hukumu kwa sasa.”

CHANZO CHA PICHA,NEGAR MOAZZAM/INSTAGRAM
Rajabian amesema kuwa kukamatwa kwake kumekuja baada ya kufanya mahojiano na BBC kuhusu albamu yake inayokuja; na kutangaza video yake inayomshirikisha mnenguaji mashuhuri kutoka uajemi Helia Bandeh.
BBC ilifanya jitihada za kuwasiliana na Wizara ya Utamaduni na miongozo ya Uislamu kwa ajili ya ufafanuzi kuhusu suala hilo, lakini haijajibu chochote.
Chini ya sheria za Iran, waimbaji na wacheza dansi wanaweza kuhukumiwa ikiwa mamlaka itajiridhisha kuwa muziki huo ”unakiuka maadili”
Wanawake wanaruhusiwa kutumbuiza kwenye hadhara ya wanawake pekee kwenye kikundi cha uimbaji au mwanamuziki mmoja mmoja, lakini ruhusa ni nadra sana kutolewa.
Si Rajabian pekee aliyekumbana na changamoto hii. Mwezi Mei mwaka jana , mwanamuziki wa kike Nezzar Moazzam alifikishwa mahakamani kwa kuimba mbele ya kundi la watalii huku akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni.
Miezi kadhaa iliyopita, mtengenezaji muziki Ali Ghamsari alipigwa marufuku kutumbuiza ”mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa” kwa kukataa kumuondoa mwanamuziki wa kike kwenye orodha ya watumbuizaji katika tamasha mjini Tehran.

Rajabian ameshawahi kufungwa mara mbili kwanza mwaka 2013, alifungwa macho na kutengwa kwa miezi mitatu.
Kisha akahukumiwa kifungo cha miaka sita katika gereza la Evin mjini Tehran. Aliingia katika mgomo wa kutokula hali iliyovutia wanaharakati wa haki za binadamu na wanaohamasisha kampeni za uhuru wa kujieleza.
Mwanamuziki huyo anasema kuwa wasanii wenzake wanaogopa kumuunga mkono na mapema mwezi huu mwanahabari wa masuala ya muziki alikamatwa na kushikiriwa katika gereza la Evin kwa siku kadhaa baada ya kutaja majina ya muziki wa wanawake na jina la Rajabian kwenye makala yake.
”Sasa msukumo uko kwangu sipaswi hata kutengeneza kazi nyingine ya sanaa hii,” alisema ”Hii inamaanisha kifo kamili cha muziki kwa ujumla, mpango wao ni kuona kazi yangu inaharibika kabisa, alisema mwanamuziki huyo.
Chanzo BBC.
The post IRAN: Mwanamuziki ashtakiwa kwa kuwashirikisha wanawake kwenye wimbo wake appeared first on Bongo5.com.