Rais wa zamani wa Inter Milan Massimo Moratti amesema anaamini Inter imekwisha anza mipango ya kumsajili mchezaji bora wa Dunia mara sita Lionel Messi kutolka FC Barcelona.


Inter Milan ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuwa zimeonyesha nia yakutaka kumsajili Messi ambaye ameonekana kusimamaia msimamo wake wa kutaka kuonda FC Barcelona pindi mkataba wake utakapo malizika.

Nohodha huyo wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina amebakikza mkataba wa mwaka mmoja na FC Barcelona ambao unamalizika june 30 mwaka 2021.

Messi ameendelea kusimamia msimamo wakutaka kuondoka baada ya Barcelona kuwa na msimu mbaya ikiwemo kuondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya kwa kipigo cha aibu cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Robo fainali lakini pia kumaliza msimu wa 2019-20 pasipo kutwaa taji lolote.



Massimo Morrati Rais wa zamani wa Inter Milan kati ya 1995 hadi 2013 anaamini Inter imeanza mipango ya Kumsajili Lionel Messi.

Morrati alikuwa Rais wa Inter Milan kati ya mwaka 1995 mpaka 2013 amesema kumuona Lionel Messi kwenye moja ya matangazo ya Televison ya kampuni ya Suning group ambao ndio wamiliki wa klabu hiyo anaamini hiyo ni ishara tosha kuwa mipango ya kumsajili Messi imeanza kufanyika.

“Sio jambo dogo hasa kiuchumi, ilo lipo wazi lakini kikwazo kikubwa na malengo ya Messi. Unapaswa kujua kama kweli anahitaji kuondoka Barclona” alisisitiza Rais huyu wa zamani wa Nerazzurri.

Inter haina mapungufu sana kwenye safu ya ushambuliaji Romelu Lukaku amekuwa na msimu mzuri ukizingatia ni msimu wake wa kwanza na Lautaro Martinez amekuwa na muendelezo bora na wote kwa pamoja wamefunga jumla ya mabao 55 msimu uliomalizika wa 2019-20.

Lionel Messi ni mchezaji bora wa Dunia mara sita hivyo hakuna timu inayoweza kumkata licha ya kuwa na umri wa miaka 33 lakini bado ni mchezaji wa kiwango cha juu.

Nerazzurri watafaidika nje na ndani ya uwanja kama wakifanikiwa kumsajili Messi, hadhi ya mahodha huyu wa Argentina itaipandisha thamani Inter Milan Sokoni na hata mvuto wa klabu utaongezeka lakini pia kiufundi ataongeza ubora kwenye kikosi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga lakini pia uzoefu alionao.

Manchester city na PSG zinaungana na Inter Milan kuwa ni miomgoni mwa vilabu vinavyotajwa kuiwinda huduma ya Lionel Messi. Lakini Manchester City wanapigiwa chepuo zaidi huenda wakinasa saini ya Messi kutokana na uwepo wa kocha Pep Guardiola ambaye aliwahi kufanya kazi na mchezaji huyo katika klabu ya Barcelona.