Baraza Kuu la CHADEMA limempitisha Said Issa Mohamed kuwa mgombea Urais wa chama hicho Zanzibar.

Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar) amepitishwa kwa kura za ndiyo na wajumbe zaidi ya 500 huku wajumbe watano wakimpigia kura za hapana.

Baraza Kuu la CHADEMA limempitisha Salum Mwalim Juma kuwa Mgombea mwenza wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Salum Mwalim ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar amepitishwa kwa kura za ndiyo na wajumbe zaidi ya 500 huku wajumbe wannne wakimpigia kura za hapana.

Salum Mwalim sasa atasubiri jina la mgombea urais atakayepitishwa na chama hicho ili aweze kuwa mgombea wake mwenza.