Wahaya walitokea Afrika Kaskazini na kupitia Uganda na hatimaye kuanza maisha katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania
Wahaya ni moja ya makabila yaliyojaliwa wanawake wazuri na wenye maumbo na shepu nzuri pamoja na tabia.
Lugha, Tamaduni,chakula (Ndizi) ya watu wa kabila hili inafanana sana na ile ya jamii ya wanyankole wa nchi jirani ya Uganda

Wahaya walianza kutambiana toka zamani na kigezo kikubwa ilikuwa ni kuwa na elimu bora “inye nsomile” maana ya “Mimi nimesoma” na huu ukawa mwanzo wa makabila mengine kuwaita “NSHOMILE
Wahaya ni mkusanyiko wa makabila saba,ambayo ni
waziba,
wahamba
wanyambo,
wanyaiyangilo,
wayoza
waendangabo
wakala.

Ni mkusanyiko kwa maana haya ni makabila kamili sio makabila madogo madogo kama watu wengi wanavyofikiria.

Hayo makabila kila moja ilikuwa ni dola kamili iliyokuwa na mamlaka kamili katika nyanja zote za kiutawala,kijamii,kisiasa kiuchumi na kijeshi.Na kila dola lilikuwa na mipaka isiyoingiliana na dola jingine na iliyolindwa barabara.

Senene ni chakula cha heshima kwa wahaya toka zama za kale

Jamii hii ilikuwa na utawala wa wa koo na mtawala mkuu aliitwa Mukama

Alitokana na ukoo maalumu uliotoa mukama kila dola ilikuwa na koo tofauti zilizizotoa Bakama,Waziba ukoo uliotoa

Bakama ni ukoo wa Babiito.Wanyambo,Wanyaiyangilo na Wahamba ukoo wa Bakama ni Bahinda.

Hawa watawala walikuwa na mamlaka kamili kila mmoja kwenye dola lake bila kutegemea mtawala wa dola jirani.Mara nyingi dola hizi zilikuwa na migogoro ya mipaka iliyopelekea kutokea vita baina ya dola moja na nyingine.

Lugha za kila kabila zilifanana sana isipokuwa kulikuwepo na tofauti kubwa katika lahaja na tofauti ya baadhi ya maneno mfano maharage waziba na wanyambo wanaita biimba na makabila mengine wanaita mpelege. Pia kuna tofauti katka mila na desturi kutoka kabila moja na kabila jingine.

Kwa asili hakuna kabila mojalinaloitwa wahaya,hili jina limeundwa na wakoloni wa kijerumani.Wamekusanya makabila saba yenye lugha, mila na desturi zinazoshabihiana wakaliita kabila mmoja wahaya.Kwa kawaida kila kabila huwa lina mtemi wake au kiongozi mkuu wa kabila kwa kabila hili lililoitwa wahaya halina kiongozi wa aina hiyo.

MAJINA YA WAHAYA

Mtoto wa kwanza anaweza kuitwa Kokubanza, kokutangilila, Lubanzibwa Kalimuna

kama mtoto angezaliwa baada ya wazazi kukaa muda mrefu bila kupata mtoto, mtoto aliyezaliwa aliitwa ama Mushumbusi, Shumbusho, Rwezaula, kukulingilila, kokumalamala au Mkaanguki

Kama baba angekufa akamwacha mke wake ana mimba, mtoto aliyezaliwa aliitwa Kabwanga wa kike, kasigwa au kashangaki wa kiume

Pacha wa kiume aliyezaliwa kwanza aliitwa Ishengoma au Kakulu wa kike aliitwa Nyangoma, Pacha wapili kama ni wakiume aliitwa Kato. Wa kike alitwa Nyakato

Mtoto aliyezaliwa akiwafuata mapacha wakiume aliitwa Kyaluzi wa kike aliitwa Mkabaluzi

Kwa wahaya mapacha si tu watoto wanaozaliwa wawili, hata mtoto mmoja anayezaliwa kwa kutanguliza miguu huitwa pacha tena huyu ndiye huitwa pacha halisi. Kwa wahaya huita ‘eilongo alikulu’

Majina mengi ya kike huanza na KOKU mfano Kokushubila, kukoshobokelwa, Kokugonza nay a kiume huanza na Ruta kama Lutakulembelwa, Lutanywana, Lutasingwa

Kuna matumizi ya herufi ya R na H katika lugha ya luhaya sijayaelewa vizuri maana katika kuongea kwa wahaya uwezi kusikia mtu anajiita muhaya utamsikia anajiita muaya, utasikia anajiita Lweyemamu sio Rweyemamu

Wanawake wa Kihaya hutakiwa kulima heka za Maharagwe kwa ajili ya matumizi ya kaya yake na hawapaswi kusaidiwa na mumewe hata kama ni heka 10

MAJANGA YALIYO WAKUMBA WAHAYA

Majanga yanayozungumziwa mara kwa mara ni vita ya Idd Amin, ugonjwa wa UKIMWI , kuzama kwa meli ya MV BUKOBA, anguko la bei ya kahawa na kwa sasa tetemeko la ardhi

Ni matumaini yangu kwamba umejifunza kitu kupitia historia hii fupi