Uongozi wa Klabu ya Yanga leo umetoa orodha ya wachezaji 14 itakaoachana nao, na wachezaji 17 ambao itaendelea nao katika msimu ujao wa mashindano.

Wachezaji walioachwa kutokana na mikataba yao kumalizika ni Mrisho Ngasa, David Molinga (pichani), Jaffary Mohamed, Tariq Seif, Andrew Vicent, Papy Tshishimbi na Mohamed Issa.

Wachezaji ambao klabu inafanyanao mazungumzo ili kusitisha mikataba yao ni Ally Mtoni, Muharami Issa, Yikpe Gislain, Ali Ali, Patrick Sibomana, Eric Kabamba na Raphael Daud.

Wachezaji wanaobaki ni;
1. Farouk Shikhalo,
2. Metacha Mnata,
3. Ramadhan Kabwili,
4. Haruna Niyonzima,
5. Lamine Moro,
6. Bernard Morrison,
7. Feisal Salum,
8. Juma Mahadhi,
9. Adeyum Saleh,
10. Said Makapu,
11. Balama Mapinduzi,
12. Deus Kaseke,
13. Ditram Nchimbi,
14. Abdulaziz Makame,
15. Paul Godfrey.

Pia Yanga ipo kwenye mazungumzo na Kelvin Yondan pamoja na Juma Abdul ili kuongeza mikataba yao.

Je, ni uamuzi sahihi au wamebugi