STAA wa muziki wa Bongo Fleva na bosi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Rajab Abdul Khahali ‘Harmonize’ au Harmo, kupitia meneja wake, amekataa malumbano ya bangi yaliyoibuliwa na mmoja wa mameneja wa lebo yake ya awali ya Wasafi Classic Baby (WCB), Sallam Ahmed Sharaff ‘Sallam SK’.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mmoja wa mameneja wa Harmo, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ amesema kuwa, ishu ya bangi kwa Harmo si ya kuzungumzia kwa sasa kwa sababu itahitaji mambo mengi kwenye hilo ikiwemo ushahidi na vitu vingine.

“Hatuko kwenye nafasi ya kuzungumzia suala hili kwa sasa, kwa sababu ni jambo ambalo litahitaji mambo mengi, ushahidi, malumbano na mambo mengine, hivyo hatuwezi kulizungumzia,’’ alisema Beauty.

Sallam SK katika mahojiano na media moja ya hivi karibuni, amefunguka kuhusiana na chanzo cha bifu lake na Harmo.

Alisema tofauti yake na Harmo ilianza muda mrefu tangu miaka mitatu iliyopita, baada ya Harmo kumtuhumu yeye na Babu Tale (Meneja wa Mondi) kuwa ndiyo waliopeleka taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba Harmo anavuta bangi.

Sallam ameeleza kwamba tangu kipindi hicho, Harmo hakuwahi kumsalimia na alikuwa akimpita kama jiwe mpaka siku ya msiba wa mke wa Babu Tale, Shamsa Kombo ‘Shammy’ ambapo alimsalimia Sallam lakini yeye aliukataa mkono wa msanii huyo.

“Mimi siyo mnafiki, kama mtu aliamua kutonisalimia na mara nyingi amekuwa akinikataa kwa zaidi ya miaka mitatu, sasa kuna haja gani ya kusalimiana naye? Ndiyo maana hata ule mkono alionipa niliukataa,’’ aliongeza Sallam akifafanua kuhusu ile ishu ya kuukataa mkono wa Harmo kwenye msiba wa mke wa Babu Tale.

Kwenye kauli hii ya Sallam ina utata ikiwa tunafahamu ya kwamba Harmo alianza rasmi muziki mwaka 2015 baada ya kusainiwa na lebo hiyo na baadaye kujitoa mwaka Jana 2019 kuamua kuanzisha lebo yake mwenyewe ambayo ni Konde Gang iliyo na maskani yake Mbezi Beach jijini Dar. Hapo kimsingi Harmonize amekaa Wasafi sio zaidi ya miaka Nne. Kipindi hicho chote tumeona Safari zote za Harmonize alikuwa na Sallam na ishu ya Bangi imekuja 2018 sasa miaka hiyo mitatu imetoka wapi ikiwa walikuwa wanasafiri pamoja??