Na Samirah Yusuph
Kufuatia agizo la serikali kwa halmashauri zote nchini la kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya kukopesha vikundi vya vijana, wanawake, na walemavu umewanufaisha walengwa na kuwainua kiuchumi.

Wanufaika hao walio katika vikundi mbali mbali vya wanawake na vijana, wameweza kuanzisha biashara mbalimbali na kujikita katika ujasiliamali hivyo kubadirisha maisha yao.

Baadhi  wanawake walio katika vikundi wameleta bidhaa zao katika maonyesho ya nane nane kitaifa mkoani Simiyu  na wameonyesha namna ambavyo mikopo hiyo imewanufaisha.

Akiongea katika maonyesho hayo katibu wa kikundi Cha Shida na Raha kutoka Wilayani Maswa Grace Kalunde, alisema wao walipata mkopo uliowasaidia kununua mashine  ya kuchakata Katani inayowasaidia kutengeneza bidhaa zitokanazo na zao Hilo.

"Tunatengeneza mikoba na mifagio ya Katani ambayo tunaiuza lakini sisi Kama sisi hatukuwa na uwezo was kununua hi mashine hivyo serikali ilitupatia mkopo wa milioni tatu," alisema kalunde.

Kalunde alisema tangu wamepata mkopo huo, wanaweza kutengeneza bidhaa na kuziuza wenyewe hivyo wanajipatia kipato ambacho kimebadirisha maisha yao.

Baadhi ya vijana waliopo katika maonyesho hayo walisema kwamba mikopo imewawezesha wao kujiinua na kujiajiri wenyewe hivyo wanaendelea kunufaika na mikopo hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wa Tumaini la vijana kutoka kata ya Jija wilaya ya Maswa Sayayi Leonard alisema, mikopo hiyo imepanua wigo was kuendesha shughuri zao.

"Tunafanya shughuri za ushonaji wa nguo na vitambaa kabla ya mkopo tulikuwa hatujiwezi kiuchumi lakini Sasa tunafanya kazi vizuri kea sbabu tuna fedha zinazopelekea tuwezesha," alisema Sayayi.

Saba Kashilimu ni afisa kilimo wa wilaya ya maswa, alisema wao wanahamasisha wafugaji wa kisasa ili wapate faida kutoka kutoka kwa mifugo wao.

"Tunawashauri kuwa na mifugo michache ili wawafuge kisasa pamoja na kuachana na ufugaji wa mazoea ambao hauna faida," alisema Kashilimu.

Alisema wamewaelekeza wafugaji hao kuwapa lishe bora mifugo hatua iliyo Leta manufaa kwa sababu faida inaonekana.

Mratibu wa maonyesho ya nane nane wilaya ya maswa Mabula Yohana alisema, ni wakati wa watu wengi zaidi kujifunza kupitia vikundi vilivyofanikiwa ili na wao wanufaike na mikopo hiyo.

"Hapa hawaonyeshi namna wanavyo fanyakazi na bidhaa zao lakini pia wanaonyesha namna ambavyo mikopo inamanufaa," alisema Mabula.

Akiainisha namna ambavyo serikali imewawezesha wajasiriamali hao Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya  maswa  Rodgers Lyimo, alisema wametoa mafunzo ya kuwawezesha kumiliki  biashara.

"Tumewafundisha kuandaa mpango biashara, usimamizi wa fedha, kuandaa mchanganuo wa mapato na matumizi, na uendeshaji wa Vikundi pamoja na namna ya kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha" Alisema

Aidha aliongeza kuwa, Kufanya wamekuwa wakifanya usimamizi na ufuatiliaji na tathimini ya kazi zinazofanywa na vikundi vyote.

Mwisho.