Serikali ya Lebanon imetangaza wiki mbili za hali ya hatari, ambapo jeshi limepewa madaraka kamili, katika wakati huu uchunguzi ukiendelea, kufuatia mlipuko mkubwa kwenye bandari ya Beirut uliouwa hadi sasa watu 135.

Beirut has suffered a catastrophe that will live long in the ...

Bandari iliyolipuka

Kwenye hotuba yake kwa taifa hapo jana, Rais Michel Aoun alisema msiba huo hauna maelezo. Waziri Mkuu Hassan Diab ametangaza pia siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo.

Beirut explosions: Devastating photos from Lebanon show ...

Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba uzembe ndio uliosababisha mlipuko huo jioni ya Jumanne. Zaidi ya watu 5,000 wamejeruhiwa na makumi ya wengine hawajulikani walipo hadi sasa.

Beirut explosions: Devastating photos from Lebanon show ...

Maafisa wanasema watu robo milioni wamejikuta wakiwa hawana nyumba zinazofaa kukaliwa, baada ya mtikisiko wa mlipuko huo kuharibu majengo na vifaa vyao vya ndani. Timu za waokowaji zimeendelea kufukuwa vifusi kuwasaka manusura, huku idadi ya waliokufa kwenye mkasa huo wa aina yake ikitazamiwa kupanda.

Two-week state of emergency declared in Beirut following ...

The post Hali ya hatari yatangazwa Lebanon, Jeshi lapewa madaraka kamili, Rais asema msiba huo hauna maelezo appeared first on Bongo5.com.