Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu atachukua fomu kesho ya kugombea urais.

Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kuwa atashuhudia kutoka kufo kuwa mgombea urais.

“Kesho muujiza wa Mungu una chukua fomu ya kugombea Urais, nitashuhudia, kutoka kifo had I kuwa mgombea Urais. Mna uliza tutashinda urais?,” aliandika Lema

“Jibu: kama tumekishinda kifo kwa uwezo wa Mungu basi urais ni kama ice cream tu. Twendeni mpaka mwanzo wa bahari