Wakati baadhi ya vyama vya siasa vikiendelea na mchakato wa kusaka mpeperusha bendera wa chama kwenye Uchaguzi Mkuu, ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo Agosti 5, 2020, inaanza zoezi la utoaji fomu za wagombea wa nafasi ya Urais katika ofisi zake zilizopo jijini Dodoma.  

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, hivi karibuni inaonesha kwamba, wagombea Urais wenye nia ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanatakiwa kufika Njedengwa jijini Dodoma kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.

Fomu za Urais zitachukuliwa kwa muda wa siku 20 kati ya Agosti 5 hadi Agosti 25, mwaka huu na watu wenye sifa ya kugombea nafasi ya kiti cha Urais ambao watakuwa wameteuliwa na vyama vyao vya siasa vyenye usajili wa kudumu