Katibu mkuu wa chama cha maoinduzi dkt.Bashiru Ally amemuambia mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho Dkt John Magufuli kuwa yeye sio mwenyekiti wa kudumu wa chama hicho wala sio rais wa kudumu wa Tanzania bali kama akichaguliwa kwenye uchaguzi ujao hii itakuwa awamu yake ya mwisho.

Akuzungumza kwenye hafla fupi ya chama hicho baada ya mgombe huyo kuchukua fomu kwenye ofisi za tume ya uchaguzi jijini Dodoma leo Agosti 6, 2020 ameongeza kuwa aina ya uongozi ya usltani awaachie anaoshindana na sio yeye.

“Hii ni temu yako ya mwisho, wewe sio mwenyekiti wa CCM wa kudumu wala sio Rais wa kudumu. Kazi ya Usultani kwenye vyama, waachie unaoshindana nao. CCM ni chama cha uongozi, unashindana na vyama vya uchaguzi” amesema Dkt Bashiru.

Rais Magufuli mara nyingi amekuwa akisema kuwa hatoongeza hata dakika moja pindi muula wake wa uongozi kwenye nyadhifa hiyo ya juu utakapo kamilika