Na Abdullatif  Yunus Michuzi Tv.

Benki ya CRDB imeendelea kutoa Semina Wezeshi kwa Mawakala wake Mkoani Kagera Juu ya namna ya kuboresha huduma zitolewazo na Benki hiyo kitengo Cha Mawakala, katika Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Agosti 19,2020.

Semina hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, imehudhuliwa na Mawakala zaidi ya 100 kutoka katika Matawi ya  Wilaya za Bukoba mjini, Muleba & Rwamishenye ikiwa ni muendelezo wa semina hizo kwa kanda ya ziwa na maeneo mengine ya Nchini.

Tangu kuanzishwa kwa huduma ya Mawakala mnamo Mwaka 2013, kwa sasa CRDB ina mawakala zaidi ya 16,000 waliotapakaa Tanzania nzima, na ina mawakala zaidi ya 400 katika Mkoa wa Kagera, hii inafanya  CRDB kuwa na mawakala wengi kuliko Benki yeyote Nchini ikiwa imetengeneza takribani  zaidi ya ajira elfu 20.

Mawakala wa  CRDB wamesaidia kuongeza huduma za kibenki kwa kuongeza muda wa wateja kufanya miamala ambapo baadhi ya mawakala wanatoa huduma kwa masaa 24.

Semina ya mawakala imelenga pia kuwakumbusha mawakala kufuata taratibu na kanuni zote za kifedha kama zinavyosimamiwa na Benki kuu. Wakala hao wamepewa Elimu kuhusiana na elimu ya utakatishaji Fedha. Sambamba na Hilo CRDB imetoa elimu ya ujasiliamali na njia nzuri zaidi ya kuhudumia wateja wa benki, pamoja na kusaidia kuongeza wateja ili wananchi waendelee kufurahia huduma zetu, pia CRDB wamewakumbusha huku mawakala hao wakikumbushwa Juu ya  kuhudumia wateja wao kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha wanatunza siri za wateja kwa uaminifu mkubwa

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Mawakala wa CRDB zaidi  akiwasihi Maqakala hao kujiongeza katika upande mwingine.

Meneja wa CRDB Tawi la Bukoba, Synden Bakari akizungumza kabla kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti kuzungumza na Mawakala wa Mkoa Kagera.

Goodluck Ruhago ~ Meneja Uhifadhi na ufanisi wa Mawakala kutoka makao makuu Dar es Salaam akiendelea kuwasiliana mada kwenye Semina na Mawakala
Meneja wa CRDB Tawi la Mulebba, Mr. Mbaga akisistiza na kutolea ufafanuzi  Jambo wakati wa maswali na majibu ndani ya Ukumbi wa ELCT Bukoba.

Baadhi ya Mawakala wa CRDB Mkoa Kagera wakiendelea Kusikiliza na kufuatilia matukio ukumbini ELCT HOTEL