Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa anamatumaini janga la corona litakomeshwa ndani ya miaka miwili.

A Scorecard for Dr. Tedros as the WHO's Director-General | Council ...

Akizungumza mjini Geneva, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema homa ya Spanish flu ya mwaka 1918 ilichukua miaka miwili kudhibitiwa.

Lakini ameongeza kuwa kuimarika kwa teknolojia ya sasa huenda haenda ikasaidia ulimwengu kudhibiti virusi ndani ya “muda mfupi”.

“Bila shaka watu wakiendelea kutangamana, watatoa nafasi kwa virusi kusambaa,” alisema.

“Lakini licha ya hayo, tuna teknolojia ambayo inaweza kukomesha hali hiyo, na elimu ya jinsi ya kukomesha maambukizi,” alisema, akisisitiza umuhimu wa “umoja wa kitaifa, mshikamano wa ulimwengu”.

Mafua ya mwaka 1918 yaliwaua watu karibu milioni 50 duniani.

Coronavirus kufikia sasa imewaua karibu watu 800,000 na wengine karibu milioni 23 kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo

Dkt Tedros pia alijibu maswali kuhusu ufisadi unaohusishwa na vifaa ya kinga binafsi (PPE) wakati wa janga la corona, na kutaja ufisadi huo kama “uhalifu”.

“Ufisadi wa aina yoyote haukubaliki,” alijibu.

“Hatahivyo ufisadi unaohusisha PPE… kwangu mimi binafsi na mauaji. Kwasababu wahudumu wa afya kufanya kazi bila PPE, tuna hatarisha maisha yao. Na pia kuhatarisha maisha ya watu wanaowahudumia.”

Japo swali linaohusiana na ufisadi liliangazia zaidi Afrika Kusini, nchi kadhaa zinakabiliwa na suala hilo.

Siku ya Ijumaa, maandamano yalifanywa mjini Nairobi Kenya kufuatua madai ya ufisadi wakati wa janga la corona, huku madaktari katika hospitali kadhaa za umma wakifanya mgomo kwa kutolipwa marupurupu na kukosa vifaa kingaA protester wears a mask which reads: "Arrest Covid millionaires"

Hali koje sehemu zingine duniani?

Siku ya Ijumaa, nchi kadhaa zilitangaza kuwa na ongezeko la juu zaidi ya maambukizi ndani ya mwezi mmoja.

Korea Kusini ilirekodi maambukizi ya 324 wapya – idadi ambayo ni ya juu zaidi ndani ya siku moja tangu mwezi Machi.

Nchi kadhaa za Ulaya pia zilishuhudia ongezeko la maabukizi.

Viwango vya maambukizi vimeongezeka mara mbili zaidi nchini Lebanon tangu kutokea kwa mlipuko mjini Beirut ambapo watu 178 waliuawa na maelfu ya wengine wengine kujeruhiwa Agosti 4.

Mkasa huo uliwaacha bila makao karibu watu 300,000 hali ambayo iliathiri sana juhudui za kukabiliana na maambukizi ya corona.

Barani Afrika viwango vya maambukizi ya kila siku vimeshuka akatika kile Mkuu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa, Dkt John Nkengasong, dametaja kuwa “ishara ya matumaini”.

Viwango vya maambukizi ya kila siku katika bara hilo vilikuwa 10,300 hii ikilinganishwa na 11,000 wiki iliyopita.

The post Corona itakomeshwa ndani ya miaka miwili – WHO appeared first on Bongo5.com.