China na Shirika la afya ulimwenguni WHO zinajadili mipango ya kubaini chanzo cha mlipuko wa virusi vya Corona, kufuatia ziara nchini humo, ya wataalamu wawili wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

Foreign Ministry Spokesperson Wang Wenbin's Regular Press ...

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya China Wang Wenbin, amewaambia waandishi habari kwamba wataalamu hao wamefanya mashauriano ya maandalizi kuhusu ushirikiano wa utafiti wa kisayansi kuhusu ufuatiliaji wa virusi, wakati wa muda wa wiki mbili walioka nchini humo, uliokamilika siku ya Jumapili.

60-70% population will get corona if vaccine is not developed ...

Mazungumzo yao yaligusia utafiti katika maeneo ya idadi ya watu, mazingira, molekyuli, ufuatiliaji wa wanyama na njia za maambukizi ya virusi vya corona, pamoja na mipango ya utafiti zaidi wa kisayansi, amesema Wang.

Virusi vya corona vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan katikati mwa China, mwishoni mwa mwaka jana, na vimehusishwa na soko la jumla la vyakula, ambako wanyama wa porini wanauzwa.

The post China, WHO kutafuta chanzo cha virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.