Katika uzinduzi huo Lissu amesema kuwa hawategemei kujitoa kwenye uchaguzi na kwamba kuanzia leo katika kila mkutano wa kampeni hoja yao kubwa itakuwa ni ya kurudishwa kwa wagombea waliondolewa bila kuwekewa masharti yoyote.
"Hatutajitoa kwenye uchaguzi, tutakachofanya kuanzia leo nchi nzima, katika kila mkutano wa kampeni hoja yetu ni wagombea wetu walioondolewa kinyume cha sheria warudishwe bila masharti yoyote na hata wa vyama vingine warudishwe", amesema Lissu.
Aidha amesema kuwa hoja zao siyo kwa wagombea wa CHADEMA tu, bali hata vyama vingine ambavyo wagombea wao wameenguliwa