Waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab, Jumatatu usiku alitangaza kujiuzulu kwa serikali yake, kufuatia shinikizo kutoka kwa raia wa nchi hiyo, ambao wamekuwa wakishiriki maandamano kwa siku kadhaa kufuatia milipuko mikubwa mjini Beirut Jumanne wiki jana, iliyosabisha maafa na hasara kubwa