AMA kweli duniani kuna mambo! Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45, ameuawa kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki, kufuatia kitendo cha kubaka mwili wa mwanawe mwenye umri wa miaka 14.


 


Mwanaume huyo mkazi wa kijiji cha Kiwanja Ndege, eneo la Mau Sammit nchini Kenya, alitenda ukatili huo siku moja baada ya mwanawe huyo kufariki dunia.


 


Kwa mujibu wa majirani wa mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hassan, mwanawe huyo aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika shule moja kijijini hapo, aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.


 


Aidha, familia na waombolezaji, walijawa na ghadhabu baada ya kumfumania mwanaume huyo akifanya mapenzi na mwili wa mwanawe, walipigwa na butwaa, jambo lililowasababisha kumpiga hadi kumuua.


 


Aidha, Chifu wa eneo hilo, Joseph Ng’eno alisema unywaji wa pombe haramu ya gongo, ulichangia pakubwa kitendo cha mwanaume huyo.


 


Kutokana na hali hiyo, Chifu Ng’eno alitoa wito kwa familia zote kuwa waangalifu katika masuala yanayowahusu watoto.


 


Kitendo hicho kiliwaacha wakazi wa eneo hilo vinywa wazi, huku familia hiyo wakilazimika kufanya tambiko kulingana na mila na tamaduni zao ili kuzuia maafa yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho.