Klabu ya Yanga ikiwa bado inaendelea sakata la Morrison wanaweza kujikuta kwenye kigingi kingine baada ya msemaji wa klabu ya Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru kuweka wazi kuwa mchezaji aliyetambulishwa na klabu hiyo hivi karibuni Kibwana Shomary bado ana mkataba na Mtibwa.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio mjini Morogoro kifaru amesema bado mchezaji huyo ana mktaba na Mtibwa na Yanga wamevunja sheria za soka nchini kwa kumtangaza Kibwana bila kuwasiliana na Mtibwa Sugar

“Nitaongea na viongozi kujua inakuje Yanga wanamtambulisha mchezaj ambaye ana mkataba na sisi maan kama sheria za soka nchini zinajulikana na zifuatwe nitapata ufafanuzi kutoka kwa wanasheria na utaratibu utafuata, bado Shomary ni mdog na yanga wameshawishi tu ndo kakubari” amesema Kifaru.