Katika harakati  za kutafuta wadhamini kwa wagombea Urais, mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe amesema wao wamepata  wadhamini katika mikoa kumi.

Amesema chama hicho kilimua kutafuta wadhamini kimya kimya ili kuepuka kuteleza licha ya vyama vingine kufanya hadharani ikiwemo chama cha upinzani CHADEMA pamoja na Chama Tawala ambacho ni tayari kimemaliza zoezi hilo.

Membe amehofia kuteleza ili asije vunja sheria na miongozo iliyowekwa na Tume ya Uchaguzi NEC hasa katika zoezi la kutafuta wadhamini ili isije kuambatana na kufanya kampeni kabla ya tarehe iliyopangwa.

‘’Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema’’, amesema Membe.

NEC inatarajia kutoa majina ya wateule wa nafasi ya Urais Agosti 25, ambapo kampeni zitaanza kufanyika Agosti 26.