Shirika la afya duniani (WHO) na kituo cha udhibiti wa magonjwa ya maambukizi cha Afrika (CDC) wameunda kamati itakayoshauri na kutoa usaidizi katika utafiti wa dawa za kienyeji kwa ajili ya matibabu ya Covid-19.

Flag Of The World Health Organization. Wrinkled Dirty Spots. Stock ...

Wataalamu katika kamati hiyo watazishauri nchi za Afrika kuhusu sayansi, usalama na ubora wa dawa za kienyeji.

Tume hiyo itaunga mkono nchi za Afrika kuhakikisha majaribio yote ya kitabibu ya dawa za kienyeji yanatimiza viwango vya kimataifa, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na WHO.

“Huku dunia ikiwa katika mbio za kutafuta tiba na chanjo dhidi ya virusi vya corona, utafiti katika dawa za kienyeji na ule wa dawa zinazotengenezwa viwandani zinazoweza kuwa na uwezekano wa kutibu Covid lazima uwe na misingi ya kisayansi ,” Mkurugenzi wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti, alinukuliwa akisema

Taarifa ya kubuniwa kwa kamati hiyo inakuja wakati nchi ya Madagascar, ambayo imekuwa ikipigia debe matumizi ya dawa ya mitishamba kama tiba ya Covid-19, ikiripotiwa kushindwa kuhimili idadi kubwa ya watu wenye maambukizi ya virusi vya corona.Waziri wa mambo ya nje waTanzania Palamagamba Kabudi (kulia) akionja dawa ya miti shamba kutoka Madagascar

Nigeria ilisema kuwa imefanya majaribio na haikupata ushahidi kwamba dawa ya mitishamba ya Madakgascar kweli inatibu.

Wakati huo huo Shirika la afya Duniani linasema kuwa zaidi ya wahudumu wa afya 10,000 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika, tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona.

WHO inasema kuwa viwango vya juu vya maambukizi vimetokana na upungufu wa vifaa binafsi vya kujikinga (PPE) miongoni mwa wahudumu wa afya

WHO imesema inahofu juu ya ongezeko hilo la maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwa wahudumu wa afya katika nchi za Afrika.

Maambukizi miongoni mwa wahudumu wa afya ni sawa na asilimia 10 ya maambukizi yote duniani kwa ujumla.

Wahudumu wa afya wanaowahudumia moja kwa moja wenye maambukizi ya virusi wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kisaikolojia na kimwili kwa pamoja.

Afrika Kusini, Algeria, Ghana, Ivory Coast, Cameroon, Zambia na Kenya ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya wahudumu wa afya waliopatikana na Covid-19

Wengi miongoni mwa wale walioathirika ni wauguzi. Hukaa muda mrefu wakiwahudumia wagonjwa katika wodi.

WHO imetaja sababu chache zinazosababisha kupanda kwa idadi ya maambukizi ikiwa ni pamoja na kutopatikana ipasavyo kwa vifaa vya kujikinga-au PPE, udhaifu wa hatua za kuzuwia maambukizi katika hospitali, na kulazimishwa kwa wahudumu wa afya kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19 moja kwa moja bila kupewa mafunzo stahili.

Zaidi ya watu 700,000 wameripotiwa kupata maambukizi ya virusdi vya corona huku vifo zaidi ya vya ugonjwa huo vikiripotiwa barani Afrika.

The post WHO, Afrika waunda kamati ya kutafiti dawa za kienyeji kwa ajili ya tiba dhidi ya Corona appeared first on Bongo5.com.