Kesi ya ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu itaanza tena mwezi Januari.

Indicted Israeli Prime Minister Netanyahu Fights for His Political ...

Hayo ni kwa mujibu wa uamuzi ambao umetolewa leo na mahakama ya Jerusalem ambayo pia imeeleza kuwa kila wiki mahakama itakuwa na vikao vitatu vya kusikiliza ushahidi.

Haikubainika mara moja iwapo Netanyahu atahitajika kuhudhuria vikao vyote ijapokuwa baadhi ya mashirika ya habari yameripoti kuwa atahudhuria.

Ratiba ya mahakama itayafanya masaibu ya kisheria ya Netanyahu kukita katika gumzo la kitaifa na kuendelea kuibua maswali kuhusu iwapo anaweza kuendelea kuhudumu katika serikali huku akikabiliwa na kesi hiyo.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa baada ya kikao cha pili cha kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mara ya kwanza mnamo mwezi Mei baada ya kucheleweshwa kwa miezi miwili kutokana na janga la virusi vya corona.

Netanyahu ameshtakiwa kwa udanganyifu, uvunjifu wa uaminifu na kukubali rushwa.

The post Waziri Mkuu Israel akabiliwa na kesi ya ufisadi  appeared first on Bongo5.com.