Polisi mjini Chicago nchini Marekani wamekabiliana kwa risasi za mpira na kisha kuwakamata waandamanaji kadhaa waliojaribu kuiangusha sanamu ya mpelelezi wa kizungu wa karne ya 15 Christopher Columbus.

Eighteen cops injured & 12 protesters arrested after violent ...

Makabiliano hayo yalizuka wakati kiasi watu 1,000 walipojaribu kuiparamia kwa lengo la kuiangusha sanamu ya Columbus muda mfupi baada ya kumalizika maandamano ya kuwaunga mkono watu weusi na wakaazi wa asili Polisi imesema maafisa wake 18 wamejeruhiwa baada ya waandamanaji kuwashambulia kwa kutumia mawe na vifaa vingine na kwamba karibu waandamanaji 12 wamekamatwa katika makabiliano hayo.

Waandamanaji karibu kote nchini Marekani wametoa wito wa kuondolewa kwa sanamu za Columbus, wakisema mpelelezi huyo wa kitaliano anahusika na mauaji na unyonyaji uliofanywa dhidi ya wakaazi wa asili wa bara la Amerika.

The post Waliotaka kuliangusha sanamu la mpelelezi wa karne ya 15 watiwa mbaroni appeared first on Bongo5.com.