Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Kagera inawashikilia walimu watatu  wa shule ya Sekondari Kalenge Day iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kwa kufanya udanganyifu.
 
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha april –june mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph julai 6 mbele ya waandishi habari ofisini kwake amesema walimu hao wanashikiliwa kwa kujihusisha na makosa ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi na kufanya usajili kwa udanganyifu.

Amesema katika zoezi la ufanyaji wa mtihani wa  taifa kidato cha nne  mwaka 2019  watuhumiwa hao walifanya udanganyifu kwa kumfukuza mwanafunzi  mmoja shule na kumuingiza  mwanafunzi mwingine kupitia namba ya usajili ya mwanafunzi huyo aliyefukuzwa.
 
Bw.Joseph amesema kuwa baada ya matokeo ya mtihani huo kutoka mwanafunzi ambaye hakufanya mtihani alishangaa kuona matokeo ya kionyesha amepata divison 2 na ndipo mzazi wa mwanafunzi huyo pamoja na mwanafunzi walipo toa taarifa TAKUKURU  tarehe 16/06/2020.
 
Kadhalika bwana joseph amesema kutokana na uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU mkoani Kagera,ulibaini kuwa wapo walimu watatu ambao ni pamoja na Boniface Eliabi mkuu wa shule hiyo,Edwin Valentin ambaye pia ni makamu mkuu wa shule hiyo pamoja na mwalimu Gedivas Richard  walioshilikiana kufanya udanganyifu huo na wote wanashikiliwa na uchunguzi unaendelea na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.