Inadaiwa kuwa wachezaji wa Barcelona wanamtaka aliyekuwa nyota klabu hiyo Patrick Kluivert kukabidhiwa mikoba ya Quique Setien ili kuwa kocha mpya wa timu hiyo na hii ni kwa mujibu wa gazeti la habari za michezo la la Hispania, Mundo Deportivo limedai kuwa.

Barcelona's dressing room want former player Patrick Kluivert as their new manager

Kocha Mkuu wa Barcelona, Quique Setien kwa sasa yupo katika presha kubwa juu ya kibarua chake baada ya kushindwa kulinyakua taji la LaLiga na kushuhudia likienda kwa hasimu wao Real Madrid.

Kluivert ambaye ameifungia Barcelona jumla ya magoli 122 katika michezo yake 256 aliyoitumikia klabu hiyo kwa sasa ni ‘academy director’ ndani ya Barcelona.

The club's current head coach Quique Setien is under increasing pressure at Barcelona

Baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Uholanzi kutundika daluga akawa Kocha Msaidizi wa klabu ya AZ Alkmaar na NEC Nijmegen.

Kisha baada ya hapo akawa Kocha Mkuu wa klabu ya FC Twente na kuwasaidia kutwaa kombe la ligi.

Kluivert kisha akawa Kocha msaidizi wa Louis van Gaal ndani ya timu ya taifa ya Uholanzi na kusaidia kufika hatua ya tatu bora kwenye michuano ya kombe la Dunia mwaka 2014.

Baada ya hapo akawa Kocha Mkuu wa Curacao national kabla ya kuelekea Ajax. Kisha akawa Mkurugenzi wa soka pale Paris Saint-Germain na kuachana nao kabla hata ya ujio wa Neymar uliyovunja rekodi ya usajili wa paundi milioni 200.

Amekuwa Barcelona academy director tangu Julai mwaka 2019 na amekuwa akikubalika mno kwa wachezaji wa klabu hiyo.

Wachezaji wa Barcelona wanaamini nyota huyo ambaye alikipiga ndani ya klabu hiyo kwa mafanikio makubwa ataweza kuipatia timu na mchezaji bora duniani Messi kile wanachohitaji.

The post Wachezaji Barcelona wamtaka Patrick Kluivert appeared first on Bongo5.com.