Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mhe. Dr.Phillis Nyimbi amesema masuala ya usalama na afya kwa wajasiriamali ni muhimu, kwani kutokuzingatia kwake kuweza kuleta athari kwa mfanyakazi na hivyo kutaathiri jamii na taifa kwa ujumla.

Mhe. Nyimbi amesema hayo wakati akifungua Semina maalumu kwa wajasirimali wadogo na wakati ya usalama na afya yalioyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na SIDO mkoa wa Mwanza, mafunzo yaliyofanyika Jijini Mwanza. Amesema endapo tahadhari haitachukuliwa, itawasababishia madhara makubwa na hivyo kuwa mzigo kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo,Utafiti,na Takwimu, Ndugu Joshua Matiko, amesema wajasiriamali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali na hivyo kuwataka kila wanapokuwa wanafanya shughuli zao wazungumzie masuala ya usalama na afya kabla ya kuanza kazi, ili kubainisha vihatarishi vinavyopatikana kwenye maeneo yao kazi.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo, wamesema semina hiyo imewajengea msingi mzuri wa kuweza kufanya shughuli zao za uzalishaji huku wakichukua tahadhari ya kufanya kazi katika mazingira salama na kulinda afya zaa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kufungua semina hiyo, Meneja wa SIDO mkoa wa Mwanza Ndugu Bakari Songwe amesema, SIDO kama taasisi wezesheji kwa wajasiriamali amesema waliona umuhimu wakuwashirkisha OSHA kwenye semina hiyo ili kuwawezesha wajasirimali hao namna bora ya kufanya kazi huku wakizingatia Usalama na Afya wakiwa kazini.

The post Usalama na Afya kwa wajasiriamali ni muhimu – DC Nyamagana (+Video) appeared first on Bongo5.com.