Magonjwa yanayotoka kwa wanyama na kuhamia kwa wanadamu yameongezeka na yataendelea kuongezeka iwapo wanyama pori hawatalindwa mbali na kuhifadhi mazingira, Wataalam wa Umoja wa Mataifa wameonya.

Magonjwa yanayotoka kwa wanyama hadi kwa binadamu ambayo hupuuzwa huuwa watu milioni mbili kila mwaka, wamesema.

Covid-19 inatarajiwa kugharimu uchumi wa dunia takriban $9tn (£7.2tn) katika kipindi cha miaka miwili.

Kwa nini tunaambukizwa magonjwa mengi kutoka kwa wanyama?

Ebola, Virusi vya magharibi mwa Nile na Sars ni magonjwa yaliotoka kwa wanyama na kuhamia kwa binadamu.

Je wataalam hao walisema nini?

Maambukizi hayo kutoka kwa wanyama hadi kwa bindamu sio ya moja kwa moja.

Husababishwa, kulingana na ripoti ya shirika la mazingira katika umoja wa mataifa na taasisi ya kimataifa kuhusu utafiti wa mifugo, kwa kuharibu mazingira asilia – kwa mfano kupitia uharibifu wa ardhi, utumiaji mbaya wa wanyamapori, uchimbaji wa rasilimali na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hii inabadilisha jinsi wanyama na binadamu wanaingiliana.

A lone man and a cow are seen by a submerged house after a dam collapse in Minas Gerais, Brazil. Photo: January 2019

”Katika karne iliopita, tumeona milipuko sita ya virusi vya corona”, alisema Inger Andersen , katibu na mkurugenzi mkuu katika shirika la Umoja wa mataifa kuhusu mazingira.

Katika kipindi cha miongo miwili na kabla ya Covid-19, magonjwa yanayotoka kwa wanyama yalisababisha uharibifu wa kiuchumi uliogharimu $100bn (£80bn).

“Alisema kwamba watu milioni 2 katika mataifa yenye kipato cha chini na yale ya kipato cha kati hufariki kila mwaka kutokana na kupuuzwa kwa milipuko inayotokana na wanyama kama vile Anthrax, kifua kikuu cha wanyama na kichaa cha mbwa.

Hizi ni jamii zilizo na matatizo ya kimaendeleo na hutegemea sana mifugo na ukaribu wa wanyama pori.

”Utumiaji wa wanyama pori kwa lengo la kupata nyama kwa mfano umeongeza tatizo hilo kwa asilimia 260 katika kipindi cha miaka 50”, alisema Bi Andersen.

”Tumeimarisha kilimo, kupanua miundo msingi na kuchimba mali asili bila ya kuwajali wanyama pori”, alielezea.

Mabwawa, unyunyizaji na viwanda vinahusishwa na asilimia 25 ya magonjwa miongoni mwa binadamu.

Usafiri, uchukuzi na usambazaji wa vyakula umefutilia mbali mipaka na umbali.

Mabadiliko ya hali ya anga yamechangia kwa kusambaa kwa viini vinavyosababisha magonjwa.

Ripoti hiyo inatoa mikakati kwa serikali kuhusu jinsi kuzuia milipuko ya siku zijazo, kupitia kuhamasisha usimamizi endelevu wa ardhi, kuboresha maisha miongoni mwa viumbe tofauti na uwekezaji katika utafiti wa kisayansi.

”Sayansi iko wazi kwamba iwapo tutaendelea kutumia wanyamapori na kuharibu mazingira , basi tutarajie milipuko ya magonjwa kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu siku za usoni”, alisema bi Andersen.

Ili kuzuia milipuko katika siku zijazo, ni muhimu kulinda mazingira.

The post UN yaonya, Tutakumbwa na milipuko zaidi iwapo tutaendelea kula wanyama pori appeared first on Bongo5.com.