Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amemkaribisha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM Bernard Membe, kuunganishe nguvu kupitia vyama mbadala hii ni mara baada ya yeye kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.


Kushoto ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na kulia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho hii leo Juni 30, 2020, ambapo imeandikwa hivi,

“Ndugu yangu Bernard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM, ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala” umeeleza ujumbe huo ambao umetolewa na Zitto Kabwe.

"Mimi najua @BenMembe anaipenda Tanzania na ni Mwana demokrasia.
Adhihirishe mapenzi yake kwa nchi yetu kwa kuongeza nguvu kwa vyama mbadala."@zittokabwe
Kiongozi wa Chama pic.twitter.com/kD6E7XHTDS

— ACT Wazalendo (@ACTwazalendo) June 30, 2020

OPEN IN BROWSER