Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UJENZI wa Mradi wa Maji wa Mkuranga umefikia asilimia asilimia 80 unaendelea kutekelezwa kwa kasi ili kukamilika kwa wakati na wananchi kuanza kupata huduma ya maji safi.
Mradi huo unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam DAWASA unahusisha ujenzi wa tanki la lita milioni 1.5 na ulazaji wa mabomba ya usambazaji.