Dawa ya Udanol iliyotengenezwa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambayo imerahisisha badala ya kutumia majani ya miti shamba tofauti, lakini yenyewe imetengenezwa kwa mtindo wa miti hiyo hiyo ila kwa kutoa mafuta ya miti mbalimbali na kuiongezea dhamani zaidi.
Meneja Mradi wav dawa ya Udanol, Stephen Nyandoro akizungumza na mwandishi wa Michuzi Blog katika Maonesho ya Kibiashara ya 44 katikaviwanja vya maonesho vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu Saba saba.
 CHUO kikuu cha Dar es Salaam chatengeneza dawa ya kujifukiza (Nyungu) ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa kisasa zaidi amapo hutumii majani ya miti lakini unatumia mafuta tete.

Akizungumza na Michuzi Blog Meneja mradi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Stephan Nyandoro amesema kuwa dawa ya kujifukiza ijulikanayo kama Fukiza 'Udanol' imetengenezwa kwa miti mbalimbali yenye kutoa mafuta ambayo yanasaidia kuzibua mfumo wa upumuaji ulioziba. 

Akizungumza katika banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam lililopo katika Maonesho ya Saba saba jijini Dar es Salaam amesema kuwa watanzania wawe na imani na dawa zinazotengenezwa kwa miti shamba hapa nchini kwani zinatibu.

"Dawa hii imetoka na mimea ambayo jamii yetu imekuwa ikitumia kwa kujifukiza kwaajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayoshambulia mfumo wa upumuaji, sasa sisi tumeona watu wanatumia majani na  magome kwaajili ya kujifukiza sasa chuo chetu tukaona tutafute mbadala ambao utasaidia kupambana na ugonjwa huu wa Corona."

"Tumetengeneza ikiwa nisehemu ya mchanganyiko wa mafuta tete, ambayo ni mepesi na hayana uzito wa mafuta ya kupikia, mafuta haya yanapeperushwa kwenye hewa na ukichemsha maji yanaondoka kiurahisi.

Amesema kuwa unapoyatumia kwa kujifukiza kwa kutumia mimea mafuta tete yanayosaidia katika kutibu maradhi mbalimbali.

Amesema mafuta hayo ukitaka kutumia unachemsha maji lita moja na kuweka matone mawili au matatu tuu ndipo unaanza kujifukiza. 

Licha ya hivyo Nyandoro amesema kuwa unaweza kujifukiza kwa dakika tano hadi 10. Pia amesema mbadaka wa dawa hiyo ya kujifukiza unaweza kutumia kwenye chai kwa kuweka tone moja la dawa hiyo ya Udanol.