Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya umekanusha taarifa kuwa Ujumbe rasmi uliomuwakilisha Rais Uhuru Kenyatta katika msiba wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ulizuiwa kutua nchini.

Ujumbe huo ulioongozwa na Samuel Losuron Poghisio ulilazimika kurejea jijini Nairobi kwasababu ya hitilafu ya ndege ambapo Mamlaka za Tanzania zilipewa taarifa.

Ubalozi umesema taarifa hizo za upotoshaji, za uongo na zenye lengo la kuzorotesha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya iliyotangaza siku 3 za maombolezo kufuatia kifo cha Mzee Mkapa.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kenyatta alimuelezea Rais Mkapa kama shupavu aliyetetea maslahi ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

The post Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya wakanusha taarifa ya wajumbe wa Kenyatta kuzuiliwa kutua Tanzania appeared first on Bongo5.com.