Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu yupo njiani kurejea Tanzania baada ya kuwa nje ya nchi kwa takribani miaka mitatu.

Kupitia mtandao wake wa Twitter muda mfupi uliopita, Lissu amesema kuwa anapanda ndege ya kumalizia safari yake kutoka Adis Ababa, Ethiopia mpaka Dar es Salaam, Tanzania.


Lissu aliondoka Tanzania baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa jijini Dodoma, Septemba 2017 na akakimbizwa kwa matibabu Kenya na baadaye nchini Ubelgiji.