PAPY Tshishimbi,  nahodha wa Yanga, amesema kuwa muda wowote anaweza kusaini dili jipya ndani ya klabu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael. 

Hivi karibuni ilielezwa kuwa nyota huyo amegoma kusaini dili jipya ndani ya Yanga na kuingia anga za Simba.

Miongoni mwa vitu ambavyo alikuwa anavihitaji ni pamoja na kuona timu inafanya usajili mzuri pamoja na malipo ya stahiki muhimu hasa kwa upande wa maslahi.

Tshishimbi amesema kuwa kila kitu kuhusu kuongeza mkataba kimekwenda sawa na ameona ni bora aendelee kubaki ndani ya Yanga.

"Kila kitu kipo vizuri na nimezungumza na uongozi tumekubaliana muda wowote kuanzia sasa nitasaini mkataba kwa sababu viongozi wameniambia msimu ujao mambo yatakuwa mazuri," amesema.