Rais Donald Trump ametishia kutuma maafisa wa jeshi katika miji mingi zaidi Marekani kudhibiti maandamano yanayoendelea.

Supreme Court rejects House Democrats' plea to speed up Trump tax case

Bwana Trump Jumatatu amekosoa miji kadhaa inayoongozwa na chama cha “liberal Democrats”, ikiwemo Chicago na New York, akisema kuwa viongozi wanaogopa kuchukua hatua.

Trump speaking now, awaiting any comments he might make about ...

Alisema kuwa maafisa waliotumwa Oregon wamefanya kazi nzuri ya kurejesha amani huku kukiwa na siku kadhaa za maadhamano eneo la Portland.

Hata hivyo, maafisa wa eneo wamesema kuwa maafisa wa serikali wanafanya hali kuwa mbaya zaidi.

Viongozi wa majimbo wametaka Bwana Trump kuondoa maafisa alioagiza kupelekwa huko Portland na kumshutumu kwa kufanya hali kuwa mbaya zaidi kama njia ya kutafuta ushawishi wa kisiasa mwaka wa uchaguzi.

Je Trump amesema nini?

Akizungumza katika Ikulu ya Marekani Jumatatu, Bwana Trump alirejelea wito wa utekelezaji sheria na utaratibu.

“Tunatuma vikosi,” aliwaambia wanahabari. “Hatuwezi kuacha hili liendelee kutokea katika miji.”

Alitaja miji ya New York, Chicago, Philadelphia, Detroit, Baltimore na Oakland akiwa anazungumzia matatizo yatokanayo na ghasia.

“Hatuwezi kuacha hili litokee katika nchi yetu, yote ni maeneo yanayoongozwa na chama cha liberal Democrats.”

Bwana Trump pia alipongeza juhudi za maafisa hao waliosababisha utata kwa kutekeleza sheria huko Portland. Mji huo umekuwa ukishuhudia maandamano dhidi ya unyama unaotekelezwa na polisi mjini humo tangu kutokea kwa mauaji ya George Floyd, mwanaume mweusi huko Minnesota Mei.

Bwana Trump alituma maasifa wa serikali katika hilo la magharibi mwa pwani ya Marekani wiki mbili zilizopita kutuliza maandamano hayo.

Kundi la kinamama linaonekana kati kati ya waaandamanaji mjini Portland
Maelezo ya picha,Kundi la kinamama linaonekana kati kati ya waaandamanaji mjini Portland

Baadhi ya maafisa wametumia magari ya kawaida na kusababisha ukusoaji mkubwa kutoka kwa Democrats na wanaharakati.

Wiki iliyopita, wasiwasi kati ya waandamanaji na maafisa hao wa polisi umeongezeka na viongozi wa eneo wametoa wito kuwa maafisa hao wa serikali kuu waondoke mjini humo.

Bwana Trump alisema kuwa gavana wa Oregon, meya wa Portland na viongozi wengine wa majimbo wanaogopa raia hao aliowataja kama wanaopinga serikali.

“Wanaogopa watu hawa,” amesema. “Hiyo ndio sababu hawataki sisi tuwasaidie.”

Aliongeza: “[Maafisa wa serikali] wamekuwa hapo kwa siku tatu na wamefanya kazi nzuri kwa kipindi fupi tu, hakuna matatizo. Wanashika watu wengi na kuwafunga viongozi gerezani. Hao ni watu wanaoasi serikali.”

Maafisa hao ni sehemu ya idara mpya ya usalama wa ndani.

Wamepelekwa katika eneo hilo kwa agizo la rais la kulinda masanamu, lililotiwa saini na Bwana Trump mwezi uliopita. Agizo hilo linaruhusu maafisa wa serikali kupelekwa sehemu yoyote bila viongozi wa eneo kuombwa ruhusa ya kufanya hivyo.

Pia maafisa 150 wamepangiwa kupelekwa Chicago wiki hii, ili kusaidia maafisa wengine wa serikali pamoja na maafisa polisi wa Chicago kupambana na uhalifu.

Meya wa Chicago Lori Lightfoot awali alikuwa amesema ana wasiwasi kwa hatua ya Bwana Trump ya kupeleka maafisa wa serikali mjini humo. Aliongeza kuwa amezungumza na meya wa Portland Jumapili ili kupata uelewa zaidi wa kile kinachoendelea.

“Hatutaki maafisa wa serikali bila taarifa zozote wanaochukua watu barabarani na kuwakamata, nafikiri hilo ni kinyume cha sheria,” Bi. Lightfoot amesema.

Akizungumza na CNN Jumapili, meya wa Portland Ted Wheeler alisema kuwa ‘kuna wanajeshi kadhaa ikiwa sio mamia’ mjini humo, na kuongeza: “Uwepo wao unafanya kuwe na maandamano na uharibifu zaidi wa mali.

“Hapa hawatakikani. Hatujawaomba kuja hapa. Na hasa tunachotaka ni wao waondoke,” alisema.

Aidha mwanasheria mkuu wa Oregon amewasilisha keshi dhidi ya serikali kuu kwa kuwakamata waandamanaji kinyume cha sheria na kukiuka haki ya kikatiba.

The post Trump atishia kutumia wanajeshi kudhibiti maandamano Marekani appeared first on Bongo5.com.