Hushpuppi na wenzake hao walitiwa nguvuni na kikosi kazi cha polisi wa Dubai kwa ushirikiano na Polisi wa Kimataifa kwenye operesheni iliyopewa jina la Fox Hunt 2. Wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo Utapeli, Utakatishaji fedha, Udukuzi, Wizi kwenye taasisi za Kibenki na Utapeli wa mtandaoni ambapo wanadaiwa kudukua barua pepe na tovuti za mabenki kisha kujihamishia fedha kwenye akaunti zao.
Mbali na kuwakuta na pesa taslimu kiasi cha TSH. Bilioni 92.7, Hushpuppi na genge lake wanadaiwa kutapeli takribani Trilioni 1 za Kitanzania kwa watu milioni 1.9 duniani. Pia wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kuhamisha fedha kiasi cha TSH. Bilioni 81 za ununuzi wa vifaa vya Upumuaji 'Ventilators'' kutoka Serikali ya Marekani kwenda kwa raia wake waishio Afrika.