Zindzi Mandela, mwana wa rais wa zamani wa Afrika Nelson Mandela na Winnie Madikizela – Mandela, amefariki dunia kwa mujibu wa chombo cha habari cha taifa hilo SABC.

Zindzi amefariki mjini Johannesburg mapema Jumatatu akiwa na umri wa miaka 59. Kifo chake kimethibitishwa na chanzo kimoja cha familia, kimesema chombo cha habari cha SABC. Alikuwa balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark. Amewaacha nyuma watoto wanne na mumewe.

The post TANZIA: Mtoto wa kike wa Nelson Mandela, Zindzi Mandela aaga dunia appeared first on Bongo5.com.