Aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Boniface Maiga amefariki dunia katika ajali ya gari katika eneo la Vikonji Dodoma usiku wa kuamkia leo, wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu wa CCM jijini Dodoma.
Mnamo saa 7 usku maeneo ya Vikonji Dodoma tumempoteza DAS HANDENI Comred Boniphace Maiga katika ajali ilihusisha gari la Omari Kigoda ambaye ni Mbunge wa Handeni na Bus aina ya Tata.
Gari la Kigoda lilikua na watu wanne akiwemo Omari Kigoda, DAS, Dereva na Msaidiz wa Kigoda. Hali za wengine zinaendelea vizuri katika Hosptal ya Rufaa ya Dodoma. Mwili wa Marehemu Bonface Maiga upo Hosptal ya General. Hakika Maisha yetu ni mafupi mno.


Chanzo Eatv.tv
The post TANZIA: Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Handeni Boniface Maiga afariki dunia kwa ajali ya gari akielekea Dodoma appeared first on Bongo5.com.