Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara inawashikilia watu 5 ambao ni wajumbe wa mkutano wa mkoa wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa wagombea ubunge viti maalumu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Mara, Alex Kuhanda amesema taasisi hiyo licha ya kukamata wajumbe  hao pia imekamata kiasi cha Pesa Tsh. 3,300,000 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe ili kuhujumu zoezi la kupiga kura.

Mkuu  huyo wa TAKUKURU ameeleza kuwa kwenye kiasi hicho cha fedha kuna Tsh. 70,000 ambayo mmoja wa wajumbe aliitupa chooni baada ya kugundua mtego aliowekewa.

TAKUKURU inatarajia kuwahoji wagombea Ubunge viti Maalum 6 Mkoani Mara ambao wanadaiwa kuwa ni vinara wa kutoa rushwa katika Uchaguzi.