Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi amesema msafara uliobeba viongozi wa chama chicho leo kwenda kwenye shuguli ya kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ulichelewa kufika uwanjani hapo ndio maan ulizuiliwa kuingia.

Mbilinyi ametoa taarifa hizo leo kupita ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter na kutaka vingozi wa chama hicho waache kupiga kona okna juu ya swala hilo.

“Nilitaka kukaa kimya nisiandike kitu ila nafsi inakataa. Leo tumechemka! Viongozi wangu tusipige kona kona tulichelewa uwanjani tusije tukapata laana bure” ameandika Mbilinyi.

Mapema leo asubuhi taarifa ziliendea kwenye mitandao ya kijaii zikidai kuwa polisi waliwazuia viongozi wa chama hicho kuingia kwenye shuguli hiyo bila sababu yoyote.