Mwanafamilia William Erio akielezea sababu ya kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa.

“Napenda kutumia fursa hii kueleza kuhusu mzee wetu alikuwa na ugonjwa wa Malaria siku ya Jumatano ambapo Alhamis akaendea vizuri na baadae kunipa maelekezo nipeleke kwa kiongozi wa kiroho na baadae nikafanya hivyo.

Baadae akawa anaangalia taarifa ya habari kuhusu uchaguzi wa kura za maoni za wakina mama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye vyombo vya habari.

Sababu ya kifo alipata mshtuko wa moyo tuwaombe Watanzania wote tumuenzi na kumuheshimu mzee wetu kwa ukweli huo na hicho ndicho chanzo cha kifo chake na si vinginevyo” William Urio, Msemaji wa familia ya Mzee Mkapa

 

The post Sababu ya kifo cha Rais mstaafu hayati Benjamin Mkapa (+Video) appeared first on Bongo5.com.