Rais wa Urus Vladimir Putin ameshinda kura ya maoni ambayo itamuwezesha kubakia madarakani hadi 2036

Putin mwenye  umri  wa  miaka  67, amekuwa  madarakani kama rais na  pia  waziri  mkuu  kwa  miongo  miwili  na  kwa  hivi  sasa  ni  rais aliyedumu  nchini Urusi kwa  kipindi  kirefu  zaidi

Kura ya maoni ilitaka  kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba ambayo  yatamuwezesha Putin  kugombea  tena  katika  uchaguzi mara  mbili  zaidi  na  kuweza  kubakia  madarakani  hadi  akiwa  na umri  wa  miaka  83. Muhula  wake  wa  hivi  sasa  unamalizika miaka  minne  ijayo. Mwenyekiti wa  tume  ya  uchaguzi  ya  Urusi Ella Pamfilova  amesema.

Putin amejijengea umaarufu  kuwa  ni  mlinzi na  kiongozi  anayeweza kuleta  uthabiti  nchini humo, kinyume  na  hali  ya  kuyumba kwa uchumi na  kisiasa  katika  kipindi  baada  ya  iliyokuwa  jamhuri  ya kisovieti  katika  miaka  ya  1990 ambayo  imekuwa  kabla  ya kuingia  kwake  madarakani.

-DW