Rais wa Gambia Adama Barrow amejitenga baada ya makamu wa rais kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona

The Gambia's President Barrow enters self-isolation after deputy ...

Rais Barrow atajitenga kwa muda wa wiki mbili. Taarifa iliyotoka Ikulu ya taifa hilo zinasema makamu wa rais Isatou Touray amekutwa na virusi vya corona.

Bi Touray alisema yuko katika hali nzuri na ataenda karantini. Ikulu ya Gambia iliandika katika ukurasa wake wa Twitter

Mpaka sasa Gambia imethibitisha kuwa na watu 326 walio na maambukizi ya corona na vifo vinane vilivyotokana na maambukizi hayo.

Serikali imekuwa ikiwasisitiza wananchi kuvaa barakoa na kukaa kwa umbali hatua tatu kila mtu ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

The post Rais wa Gambia kujitenga baada ya makamu wake kukutwa na Corona appeared first on Bongo5.com.