Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ameambukizwa tena virusi vya corona, lakini amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa yuko salama.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amesema amefanya vipimo vya pili na kugunduliwa kuwa angali ana virusi vya corona.

Mnamo siku ya Jumanne, Rais Bolsonaro aliye na umri wa miaka 65, na ambaye pamoja na serikali yake wamekuwa wakipuuza makali ya ugonjwa wa COVID-19 kwa miezi kadhaa, alisema alifanya vipimo tena na kugunduliwa kuwa angali ana virusi hivyo.

Brazil imerekodi maambukizi milioni 2 ya COVID-19, hivyo kuwa taifa la pili baada ya Marekani miongoni mwa nchi ambazo zimeathiriwa zaidi.

Vile vile zaidi ya watu 75,000 wamefariki nchini humo kutokana na virusi hivyo vya ulimwenguni kote.

Wataalamu wanadhani kwamba huenda idadi ya maambukizi yako juu zaidi, katika taifa hilo lenye jumla ya watu milioni 210.

Awali Bolsonaro hakutaka kuvaa barakoa. Alihimiza uchumi wa taifa hilo kufunguliwa licha ya janga la corona, akihoji kuwa ugumu wa kiuchumi unaweza kusababisha vifo zaidi.

Mataifa mengi yamelazimika kusitisha mipango yao ya kuondoa vizuizi vya kuepusha virusi hivyo kusambaa zaidi.

The post Rais wa Brazil Jair Bolsonaro aambukizwa Corona appeared first on Bongo5.com.