Rais Magufuli ameonesha kuguswa na kifo cha aliyekuwa miongoni mwa Mawaziri 11 wa kwanza wa Tanganyika, Balozi Job Lusinde, na kuwapa pole wanafamilia wote, huku akieleza ni kwa namna gani ataukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa.

Rais Magufuli ametoa salamu hizo za pole, kupitia ukurasa wake wa Twitter hii leo Julai 8, 2020,

"Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde, nawapa pole familia, wana Dodoma na Watanzania, nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee wa Dodoma, Pumzika salama mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri" ameandika Rais Magufuli.

Balozi Mstaafu Job Lusinde, alimefariki Dunia Alfajiri ya Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila na mipango yote ya mazishi inafanyika nyumbani kwake jijini Dodoma.