Leo Julai 7, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa DC 1 na Ma-DED 5 akiwemo, Lauteri Kanoni kuwa DC wa Wanging’ombe. Aidha amemteua Bashir Mhoja kuwa Mkurugenzi Wilaya ya Iringa, Ramadhan Possi kuwa DED Chalinze pia amemteua Baraka Zikatimu kuwa DED Wilaya ya Urambo.

Pia Rais Magufuli amemteua John John Nchimbi kuwa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Babati pamoja na Emmanuel Matinyi Johnson kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, uteuzi wa viongozi hao unaanza rasmi leo Julai 7, 2020.

The post Rais Magufuli afanya uteuzi wa Ma-DED watano na DC Njombe appeared first on Bongo5.com.