Msanii na Mbunge anayeoongoza watu na wanyama Jimbo la Mikumi Prof Jay, amesema kuwa kwenye maisha haya amejifunza kuchunga sana mdomo wake kwa sababu malipo ni hapa hapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibu.

Msanii na Mwanasiasa Prof Jay ameongea hayo kupitia post aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram na Twitter na kusema kuwa, “Nimejifunza kwamba sisi wanadamu inatupasa kuchunga sana ndimi zetu, kutafakari kwa kina kauli zetu na inapobidi ni kufunga kabisa mabakuli yetu kwani malipo yapo hapa hapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibu”  kutoka kwa Prof Jay.

Tayari Prof Jay ametangaza nia ya kugombania tena kwa miaka mitano ijayo ya kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Mikumi, Mkoani Morogoro.

The post Prof Jay: Malipo yapo hapa hapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibu appeared first on Bongo5.com.